Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu hiki ”Haadi Arwaah ilaa Bilaad al-Afraah” – yaani kwenda Peponi – ambapo ndani yake mna milango mingi na miongoni mwa milango hiyo ni mlango huu wa sitini na tano. Anathibitisha – na ni haki – ya kwamba huu ndio mlango mtukufu zaidi wa kitabu hiki. Kwa sababu ni mlango unaozungumzia Pepo. Pepo imeumbwa na ndani yake mna Huur [al-´Iyn], mabustani, neema mbali mbali. Vitu vyote hivi vimeumbwa. Lakini hata hivyo kumuona Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ndio starehe ya mioyo na raha ya nafsi. Raha ya mioyo ni kitu kiko juu kuliko raha ya miili. Anasema:

”Huu ndio mlango mtukufu zaidi, wenye hadhi zaidi, ulio na khatari zaidi na kiburudisho kwenye macho ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.”

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaposoma kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya Salaf juu ya kwamba watakuja kumuona Mola wao nafsi zao zinastarehe na macho yao yanaburudika kwa kuwa wameamini kuwa watamuona Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Nafsi zao zinakuwa ni zenye kumtamani Allaah (´Azza wa Jall) na wanashindana katika ´ibaadah ili waweze kumuona Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 08-09