Swali: Mara nyingi huapa kwa Allaah kwamba wageni wetu watakula kwetu au kwamba si wao watakaolipa. Je, kuna kinachonilazimu?

Jibu: Wanazuoni wengi wanaona kwamba ukivunja kiapo chako, basi inakulazimu [kutoa kafara]. Hata hivyo Shaykh-ul-Islaam haoni hivo, kwa sababu anasema kuwa lengo ni kumkirimu, na amekwishamkirimu kwa kusema hivo. Anachotaka ni kumkirimu na ameshafanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 07/01/2024