21. Hadiyth ”Hakika Allaah anao Malaika wanaozunguka ardhini… “

21 – Musaddad ametuhadithia: Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan: ´Abdullaah bin as-Saa-ib amenihadithia, kutoka kwa Zaadhaan, kutoka kwa ´Abdullaah – Ibn Mas´uud – kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

إن لله في الأرض ملائكة سيَّاحين يبلغوني من أمتي السلام

”Hakika Allaah anao Malaika wanaozunguka ardhini wakinifikishia salamu kutoka kwa ummah wangu.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Wanamme wake ni wanamme Swahiyh. Ameipokea Ahmad, an-Nasâ’î na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” kupitia njia nyingi kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy. Cheni ya wapokezi wake imesahihishwa katika “al-Jalaa’”, uk. 27. Inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas katika “al-Kaamil” ya Ibn ´Adiy.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 36
  • Imechapishwa: 07/01/2024