Nini zinafahamisha zile Hadiyth zinazomkanushia mtu kuwa na imani?

Swali: Hadiyth zilizopokewa zenye kukanusha imani. Je, zinafahamisha kwamba aliyekanushiwa imani ametenda dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa?

Jibu: Kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni huhesabiwa kuwa ni dhambi kubwa, kama vile Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na kundi la wanazuoni wanazingatia kuwa ni dhambi kubwa, kwa sababu imani amekanushiwa imani. Mfano wa hilo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, haibi mwenye kuiba pale anapoiba hali ya kuwa ni muumini.”[1]

“Si katika sisi yule mwenye kujipiga mashavu, akachana nguo au akaita kwa wito wa kipindi kabla ya kuja Uislamu.”[2]

[1] al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Iymaan” (38) na (72).

[2] al-Bukhaariy (1294) na Muslim (103).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25254/على-ماذا-تدل-الاحاديث-التي-فيها-نفي-الايمان
  • Imechapishwa: 22/02/2025