Swali: Salafiyyah ni nini na una maoni gani juu yao?
Jibu: Salafiyyah ni unasibisho wa Salaf. Salaf ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maimamu wa uongofu kutoka katika zile karne tau bora za kwanza (Radhiya Allaahu ´anhum). Watu hawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudia wema pale aliposema:
“Watu bora ni wa karne yangu, kisha wataofuatia, kisha wataofuatia. Halafu baada ya hapo watakuja watu ushuhuda wa mmoja wao utashinda kiapo chake na kiapo chake kitashinda ushuhuda wake.”
Ameipokea Imaam Ahmad katika “al-Musnad”, al-Bukhaariy na Muslim.
Salafiyyuun ni wingi wa ´Salafiy`. Salafiy ni unasibisho wa Salaf na tumetangulia kutaja maana yake. Ni wale wenye kufuata mfumo wa Salaf katika kufuata Qur-aan na Sunnah na kulingania katika vitu hivyo na kuvitendea kazi. Kwa hayo ndio wakawa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/165-166)
- Imechapishwa: 23/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Kamati ya wanachuoni wakubwa Saudi Arabia kuhusu Salafiyyah
Swali 188: Salafiyyah ni nini? Ni yepi maoni yenu juu yake? Jibu: Salafiyyah ni unasibisho kwa Salaf ambao ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maimamu wa uongofu katika wale wa karne tatu wa mwanzo (Radhiya Allaahu ´anhum) ambao wameshuhudiwa ubora na Mtume wa Allaah (Swalla…
In "Kujiita na kuitwa ´Salafiy na Salafiyyah`"
03. Salafiyyah ni nini na nani kiongozi wake?
Swali 03: Salafiyyah ni nini? Kiongozi wake ni nani? Jibu: Salafiyyah ni unasibisho wa Salaf. Salaf ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema kuanzia wale watu waliokuwa katika karne tatu bora na waliokuja baada yao. Hii ndio Salafiyyah. Kujinasibisha kwao ina…
In "al-Fataawaa al-Jaliyyah"
62. Salafiyyah ni kitu gani?
Swali 62: Salafiyyah ni nini? Je, ni wajibu kufuata na kushikamana na mfumo wake? Jibu: Salafiyyah ni kupita juu ya mfumo wa Salaf. Salaf walikuwa Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah na vile vizazi bora. Ni lazima kwa muislamu kuwafuata inapokuja katika ´Aqiydah, ufahamu na tabia[1]. Allaah (Ta´ala) amesema: وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ…
In "al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah"