Swali: Ni nini maana ya neno (الزَّكَاة) kwa upande wa lugha na Shari´ah? Kuna mafungano yepi kati ya hayo mawili?
Jibu: Zakaah upande wa lugha ni kuzidi na kukua. Kila kitu ambacho idadi yake inaongezeka au kinakuwa kikubwa huitwa kuwa ni (الزَّكَاة).
Kwa upande wa Shari´ah neno hilo maana yake ni kumwabudu Allaah kwa njia ya kuitolea zakaah pesa fulani kuwapa watu maalum.
Mafungamano kati yake ni kwamba hata kama swadaqah udhahiri wake ni kupungua kwa mali, lakini hata hivyo athari yake ni kwamba mali hiyo baraka yake inaongezeka na kubarikiwa. Allaah anaweza kumfungulia mtu milango ya riziki kwa namna ambayo alikuwa haifikirii pale anapotekeleza yale ambayo Allaah amemuwajibishia juu ya mali yake. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ
“Na mlichotoa katika [pesa za kuwakopesha watu mpate] ribaa ili kizidi katika mali za watu, basi [hicho] hakizidi kwa Allaah. Na mlichotoa katika zakaah mnataka uso wa Allaah, basi hao [wafanyao hivyo] ndio wenye kuzidishiwa.”[1]
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
“Na chochote mtoacho katika kitu, basi Yeye Atakilipa. Naye ni mbora wa wenye kuruzuku.”[2]
Bi maana Anampa badala yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swadaqah haipunguzi mali.”[3]
Hili ni jambo lililoshuhudiwa. Wale walioongozwa katika kutekeleza yale ambayo wamewajibishiwa katika mali zao wanaona baraka katika vile wanavyovitoa na baraka vilevile katika vile vilivyobaki kwao. Huenda Allaah akawafungulia milango mingine ya riziki wanayoishuhudia kutokana na vile wanavyojitolea katika njia ya Allaah. Kwa namna hiyo kuna mahusiano kati ya maana hizo mbili.
Aidha ni kwamba zakaah ina ziada nyingine; nayo ni kwamba inamzidishia imani yule mtoaji katika moyo wake. Hakika zakaah ni katika matendo mema na matendo mema yanamzidishia mtu imani yake. Kwani Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa matendo mema ni sehemu katika imani na kwamba imani inazidi pale matendo mema yanapoongezeka na inashuka pale matendo mema yanapopungua. Isitoshe zakaah inamzidishia mtu tabia yake kwa sababu utoaji ni alama inayofahamisha ujitoleaji na ukarimu wa mtu, hapana shaka kwamba sifa mbili hizo ni nzuri na tukufu. Bali zakaah ina taathira kubwa katika kuungufua moyo, kupanua kifua, kuungaza moyo na kuufanya kuwa na faraja. Yule anayetaka kuyahisi hayo basi ajaribu kutoa. Atahisi matokeo mazuri, khaswa ikiwa kujitolea huko ni wajibu kama vile zakaah. Zakaah ni moja katika nguzo za Uislamu na misingi yake mikuu. Mara nyingi hutajwa sambamba pamoja na swalah ambayo ndio nguzo ya Uislamu.
Vilevile ni kwamba zakaah ndio kigezo kikubwa kinachofahamisha kama kweli mtu anapenda yale yaliyoko kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwani kila mmoja anapenda pesa na mtu anapojitolea kile anachokipenda kunajulisha kuwa yule anayempa kitu hicho ndiye anapendeza zaidi kwa mtu. Jengine ni kwamba manufaa ya zakaah na matokeo yake yenye kusifiwa ni yenye kutambulika zaidi pale mtu atapozingatia.
[1] 30:39
[2] 34:39
[3] Muslim (2588), at-Tirmidhiy (2029) na Ahmad (2/235).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/11-12)
- Imechapishwa: 01/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/11-12)
Imechapishwa: 01/07/2026
https://firqatunnajia.com/nini-maana-ya-neno-zakaah/