Swali: Baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa harufu nzuri haiathiri kitu donda na uvimbe na kwa ajili hiyo yule mwenye kuona kuwa harufu nzuri inaathiri basi anategemezwa juu ya yale anayoamini. Je, haya ni sahihi?
Jibu: Kanuni inasema kwamba hukumu ya kitu haithibiti isipokuwa kwa njia ya wahy au majaribio. Kwa mfano Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu nyuki:
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ
”Kisha kula kwenye kila matunda na fuata njia za Mola wako zilizofanywa nyepesi; kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbalimbali – ndani yake mna shifaa [ya magonjwa] kwa watu.”[1]
Hapo tumepata kujua kupitia wahy ya kwamba asali ni tiba. Vivyo hivyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu haba soda:
“Ni ponyo ya kila ugonjwa isipokuwa tu mauti.”[2]
Hilo pia tumelijua kupitia njia ya wahy.
Njia ya pili ni majaribio. Majaribio kama hayo yanakuwa kwa kuhisia. Ni jambo linalotambulika kuwa baadhi ya majeraha huathiriwa kwa baadhi ya manukato na sio manukato yote. Ni jambo linalotambulika kwa majaribio. Mara tu wakati mgonjwa anapogusana na manukato basi donda huanza kupona. Ni kama ambavyo tunajua kuwa baadhi ya mimea ina athari ya uponyaji tumboni au husababisha homa. Dawa zote leo ambazo hakujateremka wahy juu yake zimethibitishwa kwa majaribio. Kutokana na ninavyojua ni kwamba baadhi ya vidonda vinaathiriwa na baadhi ya harufu nzuri. Ushahidi wa hilo ni kwamba wako waangalifu na harufu nzuri hizo; mtu anakunywa kiasi kidogo tu cha kioevu cha uchungu au kuweka matone ndani ya pua zao ili harufu ile nzuri isiingie ndani kabisa ya pua. Kwa msemo mwingine ni kwamba yale ambayo tunajua kuwa ni sababu ya kuhisiwa basi hapana vibaya kuitegemea kama sababu na hiyo sio shirki. Hata hivyo haijuzu kutumia kitu kilichozuliwa tu ambacho hakina taathira yoyote.
[1] 16:69
[2] al-Bukhaariy (5687) na Muslim (2215).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/40-41)
- Imechapishwa: 01/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/40-41)
Imechapishwa: 01/07/2026
https://firqatunnajia.com/namna-ya-kuwa-na-maarifa-ya-tiba/