Nini maana ya kushuka kwa utulivu?

Swali: Nini maana ya kushuka kwa utulivu?

Jibu: Dhahiri ni kwamba ni Malaika anayeitwa Sakiynah, ambaye hukaribia na kushuka wakati anaposikia kheri na wakati wa kusikia Dhikr na baadaye anapanda. Usayd bin Hudhwayr alipomtaja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akisoma Qur-aan hali ya kuwa ana farasi na kwamba anawaogopa watoto wake ambapo akamwambia Usayd:

“Utulivu huo ulishuka baada ya kuisikia Qur-aan.”

Alikuwa akiona angani kitu kama taa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29323/ما-معنى-نزول-السكينة-في-الحديث
  • Imechapishwa: 11/07/2025