Nini maana ya kaburi lililoinuliwa/kunyanyuliwa?

Swali: Nini maana ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha isipokuwa umeiharibu na wala kaburi lililonyanyuliwa isipokuwa umelisawazisha.”[1]?

Leo tunaona makaburi mengi yameinuliwa zaidi ya shibri moja.

Jibu: Kaburi lililoinuliwa ni lile linalokuwa juu tofauti kuliko makaburi mengine. Kaburi kama hili ni wajibu kusawazishwa na mengine ili watu wasije kufitinishwa nalo. Watu wakiona kaburi hili liko juu kuliko mengine yote kuna khatari wakafitinishwa nalo. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ayasawazishe makaburi yote yaliyoinuliwa.

[1] Muslim (969).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/186)
  • Imechapishwa: 26/08/2021