Ni ipi maana ya Tarbi´ wakati wa kubeba jeneza?

Swali: Ni ipi maana ya Tarbi´ wakati wa kubeba jeneza? Je, hili lina asli?

Jibu: Tarbi´ ina maana ya kwamba jeneza linabebwa kutoka kwenye pembe zake nne. Kwanza linatakiwa kunyanyuliwa kwenye pembe la mbele upande wa kulia wa maiti. Kisha mtu aende nyuma kwenye pembe la upande wa kulia. Kisha mtu aende mbele kwenye pembe la mbele upande wa kushoto. Halafu mtu arudi nyuma kwenye pembe la upande wa kushoto. Haya yamepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah na wakayapendekeza wanachuoni. Lakini ikiwa kuna msongamano lililo bora ni mtu afanye kile ambacho ni sahali ili asijichokeshe na asiwachokeshe wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/166-167)
  • Imechapishwa: 26/08/2021