Amegundua mifupa ardhini pindi alipokuwa anajenga nyumba

Swali: Kuna mtu alikuwa anachimba msingi wa nyumba yake akakutana na mifupa akaitoa. Ni ipi hukumu ya kitendo chake hichi?

Jibu: Akiwa na uhakika au dhana yenye nguvu ya kwamba ni mifupa ya muislamu, haijuzu kuiotoa. Maiti waliyomo ndani ya makaburi wana haki zaidi ya ardhi kuliko yeye. Walipowazika wao ndio wakawa wamiliki wa ardhi. Haifai kwake kujenga nyumba juu ya makaburi ya waislamu. Akiwa na uhakika kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya makaburi ni lazima kwake kuiondoa nyumba hiyo na kuyaacha makaburi hayana nyumba yoyote. Katika hali kama hizi ni wajibu kurejea mahakamani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/213)
  • Imechapishwa: 26/08/2021