Mtu afanye nini na sehemu ya makaburi ya zamani ambapo kumegeuzwa barabara?

Swali: Mtu apafanye nini sehemu ya makaburi pa zamani ambapo kumegeuka barabara inayopitwa na watu na wanyama?

Jibu: Wale watu wa makaburi wana haki zao kwa kuwa ni waislamu. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameakataza kuyakanyaga na kukaa juu yake na kusema:

“Mmoja wenu kukaa juu ya kaa likaunguza nguo zake na likaingia mpaka kwenye ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi.”[1]

Kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza makaburi yasitwezwe amekataza vilevile yasiadhimishwe kwa njia inayopelekea katika kupetuka mipaka na shirki. Kwa hiyo amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) makaburi yasitiwe chokaa na yasijengewe na kusiandikwe juu yake.

Suala hili kuhusu sehemu ya makaburi ya zamani ambapo kumegeuzwa ni njia na barabara kwa watembeaji na magari na njia ya wanyama ni lazima lipelekwe mahakamani ili wafanye linalopasa na kuilinda sehemu ya makaburi na kujenga njia pembezoni mwake ambayo itatumiwa na watu ili kwenda kule wanakoenda.

[1] Muslim (971).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/210)
  • Imechapishwa: 26/08/2021