Nini kinachosemwa wakati wa kusindikiza jeneza?

Swali: Je, kuna Dhikr maalum kwa wale wanaoibeba jeneza?

Jibu: Sunnah ni kuwa kimya wakati wa kubeba jeneza. Sunnah ni ukimya isipokuwa ndani ya nafsi yako. Ama huyu anahimiza watu wamtaje Allaah na wampwekeshe Allaah, hii ni Bid´ah. Haina msingi. Wakati jeneza inapokuja, wanatembea wakitafakari kuhusu mwisho wa yule wa jeneza, nini ataambiwa na ni nini atajibu. Jambo ni kubwa. Kwenda kwenye mazishi na kusindikiza ni kwa ajili ya mazingatio. Kwa hiyo Sunnah kwa mwenye kuhudhuria au mwenye kusindikiza ni kufikiria na kuzingatia. Yatampata yale yaliyompata huyo wa jeneza. Atakufa kama alivyokufa. Fikiria mwisho, nini kitasemwa kwa ajili ya maiti huyu na atajibu nini. Tukio ni kubwa. Ama mtu kuwahimiza watu wamtaje Allaah na washuhudie kwake kadha na kadha, hili halina msingi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1031/ما-يقال-عند-اتباع-الجنازة
  • Imechapishwa: 08/01/2026