Nikubali posa ya mwanaume mwenye fikira za ki-Khawaarij?

Swali: Dada kutoka Tunisia anauliza. Nina binti wa shangazi yangu ambaye miaka yake imeshasogea sana, hivi sasa ana miaka thelathini na nane. Amekuja kijana anaomba amchumbie. Kijana huyu ameathirika na fikira za ki-Khawaarij na ni katika ´Awwaam na sio kichwa katika vichwa vyao. Je, akubali kuolewa nae?

Jibu: Ewe binti yangu! Moto huanza kwa cheche ndogondogo. Huyu mwanaume ambaye umenisifia, hamfai huyo dada ikiwa ni mwanamke Salafiyyah aliye juu ya Sunnah. Na wanaume wengi hujionesha kwa sura ambayo sio mpaka wanapofikia lengo lao. Wanajionesha ya kwamba watatubu, wataelekea na mwanamke huyu – Allaah akitaka – atakuwa msaidizi wake. Akishamshika barabara anamkana na kumfitinisha. Mimi simnasihi kwa hili ikiwa hali yake ni kama ulivyoelezea. Simnasihi kukubali, bali ninamtahadharisha kukubali kwa kuogopa asimfitinishe akapotea kumtoa juu ya Sunnah aliyokuwemo.

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …