Ameoa hivi punde anataka kuzuia uzazi

Swali: Ni ipi hukumu ya al-´Azl kwa aliyeoa hivi karibuni?

Jibu: Katika hekima ya ndoa ni shahawa. Na hili ni jambo ambalo mume na mke wanatakiwa kusaidizana. Na katika hekima yake vilevile ni kuzaa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

تَناكَحُوا تَناسَلُوا فإِنِّي مُباهٍ بِكم الأُمَم يَوْم القِيَامَة

“Oaneni mupate kuzaana kwa wingi, kwani mimi nitajifakharisha kwa wingi wenu juu ya Ummah wengine Siku ya Qiyaamah”.

al-´Azl ni katika sababu za kukata kizazi, na hili halijuzu. Haijuzu kukata kizazi kamwe. Isipokuwa katika hali, na hali hiyo ikithibiti kwa uchunguzi wa kidaktari ya kuwa huyo mwanamke hawezi kushika mimba kwa sababu ya maradhi yanayomzuia kufanya hivyo, kama maradhi ya moyo magumu au mfano wa maradhi kama hayo ambayo yamethibitishwa kwa uchunguzi wa kidaktari ya kuwa ushikaji wa mimba ni khatari kwake.

Lakini inajuzu kwake kupanga uzazi. Na hilo huwa pale ambapo mwanamke anazaa mbiombio. Na wala haiwezi kujulikana kuzaa kwake mbiombio isipokuwa baada ya kupata mtoto wa pili. Kwa mfano akijaribu baina ya mtoto wa kwanza na wa pili wanapishana mwaka au chini ya hapo au kumezidi [juu ya mwaka] kidogo, katika hali hii inajuzu kupanga uzazi au kupanga ushikaji wa mimba. Kwa njia ya kuwa, afanye baina ya ushikaji wa mimba mbili au baina ya watoto wawili, miaka mitatu, au miaka minne na wala asizidishe hapo. Miaka mitatu, au miaka mitatu na nusu au miaka minne inatosha. Hivyo hakuna hoja ya kuzuia mimba kwa hoja ya kwamba ndoa ni ya hivi karibuni.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/6032
  • Imechapishwa: 22/09/2020