Dadangu mume wake ana miezi miwili haswali, unamnasihi nini?

Swali: Hili ni swali la arubaini na nane. Mwanamke ana mtoto wa umri wa mwaka mmoja. Huyu mwanaume anasema, mume wa dada yake ni muislamu lakini haswali ee Shaykh, kumepita miezi haswali. Ni ipi nasaha yako kwake na ipi nasaha kwa dada yake?

Jibu: Jambo la kwanza, mfikishie dada yako na umuombe amfikishie mume wake salamu kutoka kwangu. Na kwamba sio muislamu maadamu anaacha swalah. Ikiwa atatubu na akaswali kila swalah na akahifadhi ijumaa, ni muislamu na ni mume wake. Na akikataa, atakuwa mke sio halali kwake mume na mume sio halali kwake mke, maadamu yuko katika hali hii. Mwenye kuacha swalah ni kafiri.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/6045
  • Imechapishwa: 22/09/2020