Kumpa namba ya simu mwanaume ambaye kaja kumchumbia

Swali: Je, inajuzu kumpa namba ya simu mwanaume ambaye anataka kuniposa baada ya kukubaliwa Kishari´ah ili kuelezana baadhi ya mambo?

Jibu: Tahadhari hili, ewe binti yangu. Wewe bado ni ajinabi kwake. Usiongei nae. Kukiwa na haja, mzungumzie walii wake na walii wake atamueleza. Ni wanaume wangapi nimefikiwa na khabari ewe binti yangu mambo ambayo wewe huyajui na wala watu wengi hawayajui, kwa kule kunipigia sana simu. Na mimi nasema kwamba, mwanaume mwenye kheri na mwenye msimamo hawezi kuomba namba ya simu kumuomba mwanamke ambaye si ajinabi kwake. Itapotimia kufunga ndoa, hapo ndipo utakuwa mke wake na mnaweza kujuana [zaidi kwa kuongea] na kukutembelea mara kwa mara.

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …