Nihiji tena au nimpe gharama za Hajj ambaye hajahiji?

Swali 19: Ikiwa mtu amehiji mara nyingi, je, lililo bora ni aache Hajj na atoe swadaqah kwa gharama za Hajj?

Jibu: Hili linategemea na kile ambacho haja inapelekea. Ikiwa watu wako katika haja ya swadaqah, basi swadaqah ni bora zaidi. Ikiwa hawako katika haja, basi Hajj ni bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/28)
  • Imechapishwa: 08/05/2026