Ni wajibu kufanya ´Umrah ndani ya Ramadhaan?

Swali: Baadhi ya watu wanaamini kuwa ´Umrah ni jambo la wajibu juu ya kila muislamu katika Ramadhaan. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Hili si sahihi. ´Umrah ni wajibu mara moja katika umri na halilazimiki zaidi ya hilo. ´Umrah ndani ya Ramadhaan inapendekezwa, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kufanya Hajj ndani ya Ramadhaan kunalingana na Hajj.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1863).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/35)
  • Imechapishwa: 08/05/2026