Nia katika swalah zinazopendeza maalum na zilizoachiwa

Kuhusu swalah zinazopendeza maalum; kwa mfano Witr, Dhuhaa, Rawaatib na swalah tano [za faradhi], swalah hizi ni lazima mtu azinuie kwa jina. Lakini hata hivyo kunuia ndani ya moyo na si kwa kuzitaja. Kwa mfano unataka kuswali Witr na umesema “Allaahu Akbar” lakini hukunuia kuswali Witr na ukaja kunuia kati kati ya swalah, hili si sahihi. Kwa sababu Witr ni swalah yenye kupendeza maalum. Witr maalum ni lazima mtu anuie kwa kulenga ni swalah ipi anayotaka kuswali.

Swalah zinazopendeza zilizoachiwa hazihitajii nia isipokuwa tu nia ya kutaka kuswali, jambo ambalo ni lazima. Kwa mfano mtu ametawadha na anataka kuswali Sunnah kiasi atavyokuwa amewezeshwa na Allaah. Tunasema ile nia ya swalah inatosheleza. Kwa kuwa hii ni swalah isiyokuwa maalum.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/379)
  • Imechapishwa: 24/05/2023