Nia juu ya matumizi anayotoa kuwapa familia

Swali: Ni sharti mtu aweke nia juu ya kila matumizi au atarajie malipo kutoka kwa Allaah?

Jibu:

”Hakika si venginevyo kila kitendo kinategemea na nia.”

Matendo yasiyokuwa na manuizi hayanufaishi.

Swali: Nakusudia kuwa ni imewekwa sharti mtu atarajie malipo juu ya kila matumzi au uwekaji wa nia ni mara moja?

Jibu: Hakuna haja wakati wa kutekeleza mambo ya wajibu. Atekeleze wajibu wake hata kama hakuweka nia.

Swali: Lakini anaandikiwa malipo ya swadaqah?

Jibu: Malipo ya swadaqah ni pale wakati wa kutarajia malipo kutoka kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21679/هل-تشترط-النية-والاحتساب-في-النفقة
  • Imechapishwa: 11/09/2022