Ni wakati gani inaanza du´aa katika ´Arafah?

Swali: Ni wakati gani inaanza du´aa katika ´Arafah?

Jibu: Baada ya jua kupinduka na baada ya kuswali Dhuhr na ´Aswr kwa kukusanya na kufupisha kwa adhaana moja na Iqaamah mbili. Mahujaji wataenda kiwanjani ´Arafah ambapo watatakiwa kujitahidi kuleta Adhkaar na Talbiyah. Vilevile ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwao kunyanyua mikono katika hali hiyo pamoja pia na kunza kumhimidi Allaah, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka jua litapozama.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/276)
  • Imechapishwa: 13/08/2018