Swali: Vipi mtu kufunga deni lake pamoja na kufunga swawm ya sunnah kwa nia moja. Kwa mfano kufunga siku ya ´Arafah pamoja na kulipa deni la Ramadhaan kwa nia moja?

Jibu: Ikiwa unachokusudia ni kufunga siku ya ´Arafah pamoja na kulipa deni lako, kufunga ´Aashuuraa´ pamoja na kulipa deni lako kwa maana ya kwamba ile siku ya kulipa deni lako ukaifunga siku ya ´Arafah au katika siku ya ´Aashuuraa´, hakuna neno kwako kufanya hivo na unapata thawabu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (20/49)
  • Imechapishwa: 13/08/2018