Swali: Niliswali siku ya ´Arafah Dhuhr kwa nia ya ijumaa. Lakini imamu aliswali Dhuhr. Je, swalah hii inasihi pamoja na kwamba nia ya imamu na maamuma vinatofautiana?

Jibu: Ni lazima kwako kuirudi swalah ya Dhuhr. Mahujaji hawana swalah ya ijumaa katika ´Arafah. Bali ni juu yao kuiswali Dhuhr kama alivyoiswali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/193)
  • Imechapishwa: 13/08/2018