Swali: Mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah. Nina mke ambaye bado hajahiji. Je, ni lazima kumuhijisha? Je, ni lazima kumhudumia katika hajj? Ikiwa sio wajibu kwangu hajj inaanguka kwake?
Jibu: Ampende Allaah ambaye yeye amenipenda mimi kwa ajili Yake, Allaah amjaze kheri na atufanye sisi na nyinyi tuwe katika wapenzi Wake.
Ikiwa mke alimuwekea sharti wakati wa ndoa ya kumuhijisha, basi itakuwa ni wajibu kwake kutimiza sharti hii na amuhijishe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika miongoni mwa sharti ambazo zina haki zaidi ya kutimizwa ni zile mlizohalalishiwa kwazo tupu.”
Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ
“Enyi walioamini! Timizeni mikataba.”[1]
وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا
“Timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni yenye kuulizwa.”[2]
Ama ikiwa hakumshurutishia juu yake basi sio lazima kwake kumhijisha. Lakini mimi namshauri amuhijishe kwa sababu zifuatazo:
1- Kupata thawabu. Kwa sababu anapata thawabu mfano wa zile atakazoandikiwa. Isitoshe yeye amekwishatekeleza faradhi.
2- Hiyo ni sababu ya kukoleza mshikamano wao. Kila kitu kinachosababisha wanandoa kuzidi kushikamana basi kimeamrishwa.
3- Atasifiwa na kutapwa kwa kitendo hichi.
Kwa hivyo amtake msaada Allaah na amuhijishe mke wake. Ni mamoja alimuwekea sharti juu yake au hakufanya hivo. Lakini ikiwa alimuwekea sharti hiyo basi hapo itakuwa ni wajibu kutimiza.
[1] 05:01
[2] 17:34
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1408
- Imechapishwa: 31/05/2020
Swali: Mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah. Nina mke ambaye bado hajahiji. Je, ni lazima kumuhijisha? Je, ni lazima kumhudumia katika hajj? Ikiwa sio wajibu kwangu hajj inaanguka kwake?
Jibu: Ampende Allaah ambaye yeye amenipenda mimi kwa ajili Yake, Allaah amjaze kheri na atufanye sisi na nyinyi tuwe katika wapenzi Wake.
Ikiwa mke alimuwekea sharti wakati wa ndoa ya kumuhijisha, basi itakuwa ni wajibu kwake kutimiza sharti hii na amuhijishe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika miongoni mwa sharti ambazo zina haki zaidi ya kutimizwa ni zile mlizohalalishiwa kwazo tupu.”
Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ
“Enyi walioamini! Timizeni mikataba.”[1]
وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا
“Timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni yenye kuulizwa.”[2]
Ama ikiwa hakumshurutishia juu yake basi sio lazima kwake kumhijisha. Lakini mimi namshauri amuhijishe kwa sababu zifuatazo:
1- Kupata thawabu. Kwa sababu anapata thawabu mfano wa zile atakazoandikiwa. Isitoshe yeye amekwishatekeleza faradhi.
2- Hiyo ni sababu ya kukoleza mshikamano wao. Kila kitu kinachosababisha wanandoa kuzidi kushikamana basi kimeamrishwa.
3- Atasifiwa na kutapwa kwa kitendo hichi.
Kwa hivyo amtake msaada Allaah na amuhijishe mke wake. Ni mamoja alimuwekea sharti juu yake au hakufanya hivo. Lakini ikiwa alimuwekea sharti hiyo basi hapo itakuwa ni wajibu kutimiza.
[1] 05:01
[2] 17:34
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1408
Imechapishwa: 31/05/2020
https://firqatunnajia.com/ni-wajibu-kwa-mume-kumuhijishe-mke/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)