Ni wajibu kutawadha tena kwa anayetufu wakati wa msongano mkubwa?

Swali: Je, ni lazima mtu atie upya wudhuu´ wake hata kama kuna msongamano mkubwa?

Jibu: Kwa nini?

Swali: Amepatwa na hadathi.

Jibu: Lazima afanye upya wudhuu´ wake. Ni mamoja kuna msongamano mkubwa au hakuna. Ni kama vile mtu anayevunja wudhuu´ wake akiwa kwenye swalah, analazimika kurudia swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24990/هل-يجب-الوضوء-على-من-احدث-اثناء-الطواف
  • Imechapishwa: 23/01/2025