Ni wajibu kwa ndugu zetu wajitenge mbali kabisa na maadui wa Allaah. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا

“Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui wa wazi.”  (04:101)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Enyi walioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki – wao kwa wao ni marafiki – na yeyote atakayewafanya marafiki wao, basi yeye ni katika wao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (05:51)

Ni ka nini tuko nyuma ya vyombo vya mawasiliano vya wamagharibi ambavyo vinawasifu watu kama hawa manaswara? Tunamuomba Allaah atupe sisi na nyinyi uongofu na elimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1126
  • Imechapishwa: 01/08/2020