Swali: Akiwa ana zaidi ya mke mmoja na kila mwanamke yuko katika nyumba ya kujitegemea, je, achinje Udhhiyah kwa ajili ya kila mmoja kichinjwa chake au kinatosheleza kimoja peke yake?

Jibu: Kimoja kinatosheleza. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alaiyhi wa Sallam) alichinja kichinjwa kimoja na yuko na wake tisa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanz-uth-Thamiyn, uk. 154
  • Imechapishwa: 01/08/2020