Swali: Mtu ambaye anazuia hasadi na kujionyesha yanamdhuru mambo hayo? Je, analipwa thawabu kwa kujizuilia kwake?

Jibu: Akiingiwa nafsini mwake na hasadi na asifanye wala kusema kitu hakumdhuru. Ama akifanya kitu, akamzungumza yule anayemuhusudu au akafanya kitu cha kumdhuru, basi huyu ndiye hasidi anayesemwa vibaya. Lakini asipofanya kitu, akaizuia nafsi yake na akamuomba Allaah kinga kutokamana na shaytwaan hakumdhuru.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 01/08/2020