Swali: Inafaa kuhudhuria minasaba ya kibinafsi ya Ahl-ul-Bid´ah kama ya ndoa na mingine?

Jibu: Haijuzu kuhudhuria isipokuwa kwa yule atakayeweza kukemea yale maovu yaliyomo ndani. Ama kuhudhuria na wakati huohuo mtu akanyamazia ilihali Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.” (06:68)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (99) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86-10-07-1440%D9%87%D9%80_0.mp3
  • Imechapishwa: 01/08/2020