Ni vipi mtu hutoa zakaah ya mshahara wa mwezi?

Swali: Ni jambo limeshurutishwa juu ya zakaah pesa izungukiwe na mwaka mzima. Ni vipi inatolewa zakaah ya mishahara ya mwezi?

Jibu: Pindi kunapopita mwaka mzima katika ule mshahara wa kwanza basi atoe zakaah ya ile pesa yote alionayo. Hii ndio njia bora. Ile pesa ambayo imekwishazungukiwa na mwaka mzima aitolee zakaah kwa wakati wake na ile pesa ambayo haijakamilisha mwaka basi acheleweshe zakaah yake. Kutoa zakaah kabla ya wakati wake ni sawa. Njia hii ndio bora kuliko kuchunga kila mshahara wa mwezi kivyake. Lakini hatotowa zakaah ikiwa hutumia mshahara wake kabla ya kujiwa na mshahara wa mwezi mwingine. Kwa sababu miongoni mwa sharti za kuitolea zakaah mali ni kwamba izungukiwe na mwaka mzima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/22)
  • Imechapishwa: 08/05/2021