04. Katika hali hii kuswali Rak´ah kumi na moja itakuwa bora

Maimamu wengi wa misikiti katika Tarawiyh wanaswali swalah ambayo hawaielewi na wala hawafanyi utulivu katika Rukuu´ wala Sujuud. Utulivu ni nguzo. Kinachotakikana katika swalah ni kuuhudhurisha moyo mbele ya Allaah (Ta´ala) na kuwaidhika na maneno ya Allaah yanaposomwa, kitu ambacho hakipatikani katika haraka inayochukiza.

Ingawa kuswali Rak´ah kumi na moja zilizo na kisimamo kirefu na utulivu ndio bora kuliko kuswali Rak´ah ishirini zilizo na haraka inayochukiza. Kwa sababu moyo na roho ya swalah ni kuuelekeza kwa Allaah (´Azza wa Jall). Pengine kidogo kikawa chenye kheri kuliko kingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: l-Mulakhasw al-Fiqh (01/169)
  • Imechapishwa: 08/05/2021