Ni vipi mtu ataitakasa nafsi yake na awe na nafsi yenye kutua?

 Swali: Ni zipi aina za nafsi? Ni njia ipi ya kuzitakasa kama alivosema (Ta´ala):

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا

“Hakika amefaulu yule aliyeitakasa.” (91:09)

Jibu: Aina ya nafsi zilizotajwa katika Qur-aan ni tatu:

Ya kwanza: Nafsi yenye kuamrisha sana maovu. Hii ni ile nafsi inayomwamrisha mwenye nayo yale matamanio ya haramu anayotamani na kufuata batili.

Ya pili: Nafsi yenye kujisalumu sana. Hii ni ile yenye kumlaumu mwenye nayo juu ya zile kheri zinazompiita na inamjutia.

Ya tatu: Nafsi yenye kutua. Ni ile iliyotua kwa Mola wake, ikamtii, maamrisho Yake na kumtaja na haikuelekea kwengine. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Kusema kwamba nafsi yenye kutua ni kuisifu. Kusema kwamba nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu ni kusemwa kwa ubaya. Kusema kwamba nafsi ni yenye kujilaumu ni jambo limegawanyika katika sifa na kujilaumu kwa mujibu wa yale inayomlaumu.”

Njia ya kuitakasa nafsi ni kuilazimisha kumcha Allaah (Ta´ala), kuizuia kumuasi na kuizuia na matamanio yaliyoharamishwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/fatwa/6035/%D9%85%D8%A7-%D9%87%D9%8A-%D8%A3%D9%86%D9%88%D8%A7%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%81%D9%88%D8%B3-%D9%88%D9%85%D8%A7-%D8%B7%D8%B1%D9%8A%D9%82-%D8%AA%D8%B2%D9%83%D9%8A%D8%AA%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 13/09/2018