Ni vipi kuwafunza dini watu wa kawaida na watu wa mashambani?

Swali: Watu wa kawaida na watu wa mashambani ni wengi huku kwetu. Ni vipi tutawafunza mambo ya dini yao? Tuanze kwa kitu gani?

Jibu: Wafunzeni wudhuu´, twahara, swalah na hukumu zinazohusiana na swalah. Haya ni mambo ya dharurah. Muhimu kuliko yote ni ´Aqiydah. Wafunze ´Aqiydah sahihi ijapo kwa njia ya ufupisho. Sambamba na hilo wakatazeni shirki na Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (35)
  • Imechapishwa: 29/09/2023