Ni vipi atakamilisha swalah yule aliyepitwa na baadhi ya Takbiyr za swalah ya jeneza?

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kupitwa na baadhi ya Takbiyr za swalah ya jeneza? Ni ipi hukumu ya ambaye anatoa Tasliym mbili katika swalah ya jeneza?

Jibu: Sijui Sunnah yoyote iliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi mtu atapokuja na akamkuta imamu anamswalia maiti baada ya kwamba ameshapitwa na Takbiyr moja au mbili. Lakini wanachuoni wanasema ukipitwa na baadhi ya Takbiyr iwapo jeneza litakuwa bado lipo mbele yako, kamilisha yaliyokupita kisha utoe Tasliym. Endapo jeneza litanyanyuliwa, basi katika hali hii uko na khiyari ima ya kusalimu pamoja na imamu au ukamilishe Takbiyr zako halafu utoe Tasliym. Hata hivyo sijui Sunnah yoyote juu ya hili. Anayejua Sunnah yoyote juu ya hilo basi atujuze na Allaah atamjaza kheri.

Kuhusu kutoa Tasliym mbili haina neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/135-136)
  • Imechapishwa: 15/09/2021