Ni sharti kuwepo na maafikiano wakati wa kumjeruhi mtu?

Swali: Je, ni sharti kuwepo na maafikiano wakati wa kujeruhi?

Jibu: Hii ni kazi ya wale wanazuoni wa Hadiyth. Sio sharti kuwepo na maafikiano ya kwamba mtu fulani amejeruhiwa. Anayethibitisha anatangulizwa mbele kabla ya mwenye kupinga. Ambaye anasifu ni mwenye kupinga na ambaye anajeruhi ni mwenye kuthibitisha na ndiye ambaye anatakiwa kutangulizwa mbele.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://youtu.be/IGhkGC07Amk
  • Imechapishwa: 10/11/2022