Swali: Baadhi ya ndugu wanabomoa makaburi katika baadhi ya miji ya Kiislamu kwa njia ya kuamrisha mema na kukataza maovu…

Jibu: Hili ni kosa. Hili ni kosa kubwa. Makaburi hayabomolewi isipokuwa na mtawala. Haifai kwa watu binafsi kuyabomoa. Hili husababisha shari zaidi kuliko ilioko hivi sasa. Jambo hili halifidishi kitu. Huenda likapelekea katika fitina na kuwaletea shari Ahl-us-Sunnah. Mtawala ndiye mwenye haki ya kubomoa makaburi. Zingatieni hilo!

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kufanya Hijrah alikuwa Makkah na kwenye Ka´bah peke yake kulikuwa masanamu 360 na kwenye Swafaa´ na Marwa´. Hakuyashambulia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akitufu kwenye Nyumba na akiswali na akilingania katika dini ya Allaah na hakuvamia kuyabomoa masanamu ilihali ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakufanya hivi kwa kuwa hakuna uongozi. Pindi alipohama kwenda al-Madiynah na akaiteka Makkah kwenye mikono yake kitu cha kwanza alichoanza nacho ni kuvunja masanamu. Alifanya hivi baada ya kuwa na uongozi na nguvu. Wakati huu alikuwa tayari ameshakuwa mtawala (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakuna yeyote anayeweza kuwa na kipingamizi. Hapa ndipo aliyavunja. Hii ni dalili inayoonesha kuwa masanamu na makaburi ni kazi ya mtawala wa Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf-14-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2015