Ni nani ana haki zaidi ya kumshusha maiti kaburini?

Swali: Ni nani ambaye ana haki zaidi ya kumshusha maiti ndani ya kaburi lake; msomi au ndugu wa maiti? Katika hilo kuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke? Je, imeshurutishwa yule ambaye anamshusha mwanamke awe ni katika Mahaarim zake?

Jibu: Ambaye ana haki zaidi ni yule aliyeachiwa wasia. Ikiwa hayupo basi yule ambaye yuko karibu na yeye zaidi kiudugu. Ikiwa kuna ambaye ni msomi, basi yeye ni bora zaidi afanye hivo. Na ikiwa katika wao hakuna ambaye ni msomi, basi wapokee maelekezo kutoka kwa yule msomi.

Haikushurutishwa yule ambaye anashuka ndani ya kaburi awe ni Mahaarim wa mwanamke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Abu Twalhah (Radhiya Allaahu ´anh) ashuke ndani ya kaburi na amzike msichana wake pamoja na kwamba yeye mwenyewe alikuwepo pale. Mume wa mwanamke huyu alikuwa ni ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh)[1].

[1] al-Bukhaariy (1342).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/181)
  • Imechapishwa: 24/08/2021