Ni nani aliyekwambia kuwa Fajr inamlalamikia Allaah?

Swali: Baadhi ya watoa mawaidha wanasema kuwa faradhi hii ya Fajr ni yatima ambayo inamlalamikia Allaah kutokana na wachache ambao wanaiendea?

Jibu: Maneno haya hayana msingi. Ni wajibu kusema kwamba faradhi hii watu wengi ni wazito kwayo na wanashughulishwa na usingizi. Kwa hivyo ni wajibu kumcha Allaah na kutahadhari kujifananisha na wanafiki na mfano wa maneno kama hayo mazuri. Ama kusema kwamba inamlalamikia Allaah, kunaweza kukhofiwa kwamba ni kumsemea uwongo Allaah. Ni nani aliyekwambia maneno haya?

Swali: Akemewe?

Jibu: Bora ni kuyaacha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23720/حكم-مقولة-فرض-الفجر-يتيم-يشتكي-الى-الله
  • Imechapishwa: 12/04/2024