Kuchelewa swalah kwa ajili ya kuwaandama watu kwenda msikitini

Swali: Baadhi ya maafisa wa polisi wa dini wanasema kuwa tunashughulishwa kuwatoa wanaume masokoni mpaka wanamaliza kuswali ile swalah ya mkusanyiko ya kwanza. Upande wa pili wakisema wabakie waswali na mkusanyiko wa kwanza masoko yatabaki yamejaa watu. Je, wako na udhuru wa kuchelewesha swalah?

Jibu: Ndio, wanapewa udhuru. Ni lazima kwao kuwafanya watu kuswali na mkusanyiko hata kama watakosa swalah ya mkusanyiko. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimetamani niamrishe kuswaliwe ambapo ikasimamishwa kisha nikamwamrisha mtu awaswalishe watu halafu nikaondoka na kikosi cha wanamme walio na vifurushi vya kuni kuwaendea watu ambao hawashuhudii swalah nikazichoma nyumba zao kwa moto.”

Kwa maana kwamba aondoke na kuwaacha watu huku wakiswali ili asiwashambulie na wakadai kuwa eti wamekwishaswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23719/حكم-التاخرعن-الجماعة-لاخراج-الناس-للصلاة
  • Imechapishwa: 12/04/2024