Ni lini muadhini atawaambia watu waswali katika majumba yao?

Swali: Sahihi wakati wa kusema:

ألا صلوا في رحالكم

“Zindukeni, swalini majumbani mwenu!”

ni pale anapofika katika:

حي على الصلاة

“Njooni katika swalah!”

au ni baada yake?

Jibu: Udhahiri ni kwamba atasema hivo wakati wa kusema:

حي على الصلاة

“Njooni katika swalah!”

au baada yake. Imekuja katika upokezi mwingine kwamba aliamrisha kusema hivo baada ya adhaana ili watu wasilaani wakaona kuwa adhaana imebadilishwa na adhaana ibaki kama ilivyo. Kisha awaambie:

“Swalini katika majumba yenu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23735/متى-تقال-صلوا-في-رحالكم-في-الاذان
  • Imechapishwa: 16/04/2024