Swali: Kuswali Istikhaarah inakuwa pale mtu anapokuwa ni mwenye kusita kati ya mambo mawili au ni lazima kwanza kwa mtu akate kati ya moja katika mambo mawili kisha aswali Istikhaarah katika lile ambalo tayari amekwishakata?

Jibu: Akishakata katika moja ya mambo mawili hakuna faida ya Istikhaarah. Istikhaarah inaswaliwa pale anapokuwa hajabainikiwa na kipi kilicho na manufaa zaidi [kati ya mambo mawili].

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 15/12/2018