Ni lazima kwa mwanamke kufunika miguu katika swalah?

Swali: Je, ni lazima kwa mwanamke kufunika miguu anaposwali?

Jibu: Ndio. Umm Salamah alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke anaweza kuswali na kanzu pasi na sketi?” Akasema: “Ndio, ikiwa kanzu hiyo inafunika miguu.”[1]

[1] Abu Daawuud (1/149). Ibn Qudaamah amesema: ”Wanachuoni wengi wanasema haya ni maneno ya Umm Salamah, ilihali ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdillaah bin Diynaar anaonelea kuwa ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” (al-Mughniy (2/329))
  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017