Ni lazima kwa aliyedhulumiwa kupatana na dhalimu?

Swali: Ikiwa wale ambao kati yao kuna magomvi mmoja ni dhalimu na mwengine ni mwenye kudhulumu – je, ni lazima yule aliyedhulumiwa apatane na yule dhalimu?

Jibu: Atafute suluhu na yule dhalimu na amwombe haki yake pasi na kuwa na haja ya kukatana.

Swali: Wanalingana wasipopata?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth ni kwamba ni yenye kuenea. Muda wa kuwa ni kuhusiana na haki za kidunia wasikatane zaidi ya siku tatu. Lakini ikiwa inahusiana na haki ya dini hapa ndipo inafaa…

Swali: Ikiwa yule ambaye kati yako wewe na yeye kuna ugomvi na haishi katika mji ambao wewe unaeshi. Ni vipi watasameheana?

Jibu: Utapokutana naye usimsuse. Na akiwa mbali nawe basi umestareheshwa naye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23441/هل-يلزم-المظلوم-ان-يتصالح-مع-الظالم
  • Imechapishwa: 23/01/2024