57. Hadiyth “Tumejua namna ya kukutakia amani… ”

57 – Musaddad ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Ka´b bin ´Ujrah, ambaye ameeleza:

”Wakati kulipoteremshwa Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Hivyo enyi walioamini mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”[1]

tulisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Tumejua namna ya kukutakia amani, ni namna gani ya kukuswalia?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على إبراهيم و آل إبراهيم، إنك حميد مجيد. و بارك على محمد و على آل محمد كما باركت و صليت على إبراهيم وآل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki  na kumsifu[2] Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[3]

Tunasema: ”Na sisi pamoja nao.”[4]

[1] 33:56

[2] Namna hii imekuja katika ile ya sili. Ziada hii haipatikani kwa Ahmad wala kwenye upokezi wa mtunzi unaokuja mbele. Ikiwa umethibiti katika upokezi wa kwanza, basi ni dhaifu na unaoenda kinyume. Hata hivyo imesihi kukusanywa kati ya du´aa ya swalah na baraka katika Hadiyth nyingine, isemayo:

اللهم صل على محمد و على آل محمد و بارك على محمد و على آل محمد كما صليت و باركت على إبراهيم و آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad, na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki kama ulivyomsifu na kumbariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”

Hili ndio tamko fupi zaidi lililosihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu kumsifu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni matamshi saba. Nimeyataja katika ”Swifatu Swalaat-in-Nabiy”, uk. 143-157.

[3] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Yaziyd bin Abiy Ziyaad al-Qurashiy al-Haashimiy al-Kuufiy alikuwa dhaifu kwa sababu ya kumbukumbu yake. Ahmad (4/244) ameipokea kupitia kwake.

[4] Cheni ya wapokezi ni dhaifu kutokana na yaliyotangulia kumebainishwa.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 23/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy