Ni lazima kuwaunga ndugu wa kunyonya?

Swali: Mimi nina dada zangu wa kuchangia ziwa lakini tangu utotoni mwao hawatoki kuja kunisalimia na sikutani nao. Lakini hata hivyo namtembelea mama yao ambaye anazingatiwa kuwa ni mamangu wa kunyonya. Je, dada zangu wa kunyonya wana haki ya kuungwa kizazi na kutembelewa? Je, kama siwatembelei nazingatiwa kuwa ni mwenye kukata kizazi?

Jibu: Hapana, ndugu wa kuchangia ziwa sio wa kuungwa na mambo ya kuunga kizazi hayatumiki juu yao au uwajibu wa kuwahudumia. Udugu wa kunyonya unafidisha umahram peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136
  • Imechapishwa: 12/07/2020