Swali: Kutoa thawabu za Twawaaf katika Nyumba Takatifu maiti ananufaika kwazo?

Jibu: Linahitajia dalili. Watu wanalifanya na madhehebu [ya Hanaabilah] yanaonelea kuwa ni sawa. Wanasema:

“´Ibaadah yoyote atayoifanya na akajaalia thawabu zake kwenda kwa muislamu, aliye hai na maiti atanufaika kwazo.”

Haya yanapatikana katika Zaad-ul-Ma´aad. Lakini hata hivyo linahitajia dalili ya kwamba mtu anaweza kutoa Twawaaf. Kilichowekwa katika Shari´ah ni wewe kutufu kisha umuombee maiti. Fanya Twawaaf yako mwenyewe kisha katikati ya Twawaaf umuombee maiti na kumuombea msamaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136