Ni lazima kusimama kwanza wakati wa Sujuud ya kisomo?

Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah wakati mtu anapotaka kusujudu Sujuud-ut-Tilaawah asimame kwanza?

Jibu: Sujuud-ut-Tilaawah inategemea. Ikiwa alikuwa anasoma hali ya kuwa amesimama atasujudu hali ya kuwa amesimama kwa kutokea juu. Ikiwa alikuwa anasoma hali ya kuwa amekaa, atasujudu hali ya kuwa amekaa. Na ikiwa alikuwa anasoma hali ya kuwa yuko juu ya mpando, atashutama hali ya kuwa ni mwenye kuelekea alipoelekea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015