al-Fawzaan kuhusu Takbiyr wakati wa Sujuud ya kisomo

Swali: Mtu aseme “Allaahu Akbar” ndio aende katika Sujuud-ut-Tilaawah na wakati wa kuinuka aseme “Allaahu Akbar” au asujudu bila ya kusema “Allaahu Akbar”?

Jibu: Lililothibiti ni yeye aseme “Allaahu Akbar” wakati atapoenda katika Sujuud. Ama ikiwa Sujuud-ut-Tilaawah ni ndani ya Swalah aseme “Allaahu Akbar” wakati wa kusujudu na wakati wa kuinuka. Ndani ya Swalah ni lazima alete Takbiyr. Ama ikiwa yuko anasoma nje ya Swalah aseme “Allaahu Akbar” wakati anapoenda katika Sujuud. Kuhusu wakati wa kuinuka asiseme “Allaahu Akbar”. Hata hivyo ikiwa atasema ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015