Ni kweli walii baada ya kuzikwa hupandishwa mbinguni?

Swali: Je, ni sahihi yale yanayosemwa na watu ya kwamba walii akifa na kutiwa ndani ya kaburi anajiwa na Malaika wanamtoa ndani ya kaburi hilo na kumpandisha mbinguni?

Jibu: Hilo si sahihi. Kinachopandishwa ni roho na inafunguliwa milango ya mbinguni akiwa muumini au anafungiwa nayo akiwa ni kafiri. Kisha baada ya hapo inarudishwa ardhini.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah, fatwa nr. 7781
  • Imechapishwa: 23/08/2020